TRL YASITISHA SAFARI ZA TRENI YA UBUNGO

TRL YASITISHA SAFARI ZA TRENI YA UBUNGO

Like
384
0
Wednesday, 24 December 2014
Local News

SHIRIKA la Reli la Tanzania TRL limetoa tamko la kuwajulisha abiria wote wanaotumia treni ya mjini ubungo kuwa treni hiyo imesisitisha huduma za usafiri kuanzia jana tarehe 23-29 december mwaka huu kutokana na matatizo yaliyojitokeza kwenye moja ya injini ya treni hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Afisa uhusiano wa Shirika la Reli la Tanzania TRL MOHAMED MAPONDELA amesema wanaweza kutoa huduma ya usafiri kwa injini moja ila wameona bora wazifanyie matengenezo ili warejeshe huduma yao kama kawaida.

Aidha MAPONDELA amefafanua kuwa ujio wa mabeweha ya treni ya masafa marefu kwa awamu ya pili unatarajia kuwa kabla ya kuisha kwa mwezi wa kwanza mwakani.

 

Comments are closed.