Trump aionya Iran ‘isiijaribu Marekani’, ajibizana na Hassan Rouhani

Trump aionya Iran ‘isiijaribu Marekani’, ajibizana na Hassan Rouhani

Like
677
0
Monday, 23 July 2018
Global News

Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Iran Hassan Rouhani wamejibizana vikali na kutoa vitisho huku uhasama baina ya mataifa hayo mawili ukizidi.

Bw Trump ameandika kwenye Twitter, kwa herufi kubwa, kwamba “Iran itapata madhara ambayo ni wachache sana wamewahi kukumbana nayo katika historia” iwapo itaitishia Marekani.

Bw Rouhani awali alikuwa amesema kwmaba vita na Iran vitakuwa “vita zaidi ya vita vingine vyote”.

Mwezi Mei, Marekani ilijitoa kutoka kwa mkataba wa nyuklia na Iran ambao ulikuwa umehusisha Iran kusitisa shughuli zake za nyuklia ili iondolewe vikwazo vya kimataifa.

Marekani sasa imeanza kuiwekea tena Iran vikwazo licha ya pingamizi kutoka kwa Uingereza, Ufaransa, China, Urusi na Ujerumani wote ambao walikuwa wadau katika mkataba huo wa mwaka 2015.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *