TRUMP AKEREKA MSHUKIWA WA NEW YORK KUTIBIWA NA KUPEWA WAKILI

TRUMP AKEREKA MSHUKIWA WA NEW YORK KUTIBIWA NA KUPEWA WAKILI

Like
240
0
Tuesday, 20 September 2016
Slider

Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amelalamikia hali kwamba mshukiwa anayedaiwa kutekeleza shambulio New York Ahmad Khan Rahami alitibiwa baada ya kujeruhiwa wakati wa ufyatulianaji risasi na maafisa wa polisi Jumatatu.

Aidha, amekerwa na hali kwamba mshukiwa huyo bado atapewa wakili na serikali.

Mshukiwa huyo mzaliwa wa Afghanistan mwenye umri wa miaka 28 amefunguliwa mashtaka matano ya kujaribu kutekeleza mauaji.

Bw Trump akihutubu Fort Myers, Florida amesema hiyo si “hali nzuri” na inaashiria mifumo dhaifu ya usalama wa taifa nchini Marekani. “Jambo la kusikitisha, sasa tunampa huduma nzuri sana ya kimatibabu. Atatibiwa na baadhi ya madaktari bora zaidi duniani,” Bw Trump alisema.

Comments are closed.