TRUMP APETA MAJIMBO MATANO MUHIMU MAREKANI

TRUMP APETA MAJIMBO MATANO MUHIMU MAREKANI

Like
330
0
Wednesday, 27 April 2016
Global News

NCHINI Marekani, tajiri Donald Trump amesema kuwa anajihisi sasa kama mgombea mteule wa urais wa chama cha Republican.

Amesema hayo alipokuwa akiwahutubia wafuasi wake baada ya vyombo vya habari kutangaza kuwa amepata ushindi katika majimbo yote matano kaskazini mashariki mwa Marekani.

Katika shughuli za upigaji kura wa mchujo kwenye majimbo hayo, mtafuta nafasi katika chama cha Democratic Bi Hillary Clinton alimpiku muwaniaji mwenzake Bernie Sanders, ambaye alishinda katika jimbo moja tu la Rhode Island.

Comments are closed.