TRUMP ASHAMBULIWA NA WAGOMBEA WENZAKE KWENYE MDAHALO WA REPUBLICAN

TRUMP ASHAMBULIWA NA WAGOMBEA WENZAKE KWENYE MDAHALO WA REPUBLICAN

Like
282
0
Friday, 04 March 2016
Global News

MGOMBEA Urais Donald Trump ameshambuliwa na wagombea wenzake katika mdahalo wa chama cha Republican muda mfupi baada ya wanasiasa wakongwe wa chama hicho kuwahimiza wapiga kura wasimuunge mkono.

Bwana Trump anayeongoza kwenye kura za maoni katika kinyang’anyiro cha kumtafuta mgombea wa urais wa chama cha Republican, amelazimika kujitetea vikali dhidi ya shutuma kutoka kwa Marco Rubio na Ted Cruz.

Katika mdahalo huo uliofanyika Detroit, Trump amekiri kwamba amebadilisha msimamo wake mkali lakini akasema kwamba kuweza kubadilika ni nguvu na si udhaifu.

Comments are closed.