Trump atangaza mkutano mwingine na rais Kim Jong-un wa Korea kaskazini

Trump atangaza mkutano mwingine na rais Kim Jong-un wa Korea kaskazini

Like
730
0
Wednesday, 06 February 2019
Global News

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza katika hotuba yake kwamba ataanda mkutano wa pili kujadili masuala ya nyuklia na kiongozi wa Korea kaskazini mwezi huu.

Katika hotuba kwa taifa iliyoambatana na kauli mbiu “Choosing Greatness”, aliapa kwa mara nyingine kujenga ukuta mpakani.

Huku akihimiza umoja, kiongozi huyo wa Republican pia amesema jitihada za ‘uchunguzi ulio na upendeleo’ wa Democratic huenda ukaathiri ustawi wa Marekani.

Kwa ukali, wanachama wa Democrat wamemshutumu Trump kwa kupuuza maadili ya Marekani.

Hotuba hiyo kuu ya rais Trump imejiri baada ya pengo la muda mrefu kuwahi kushuhudiwa katika historia, la kusitishwa ufadhili kutoka kwa serikali ya nchi hiyo.

Alichochea kufungwa kwa mashirika ya serikali kwa kuitisha ufadhili wa ukuta wa mpakani kati ya Marekani na Mexico na kuishia kubadili kauli hiyo baada ya wanachama wa Democrat kukataa wazi.

Amesema nini kuhusu Korea kaskazini?

Trump amesema atakuna na Kim Jong-un huko Vietnam kuanzia Febrauri 27-28.

Mipango ya mkutano wa pili imekuwa ikipangwa tangu mwaka jana.

Mnamo Jumanne usiku, Trump alisema: “Mateka wetu wamerudi nyumbani, majaribio ya nyuklia yamesitishwa na hakujakuwa na shambulio la makombora kwa miezi 15.

“Kama sikuchaguliwa rais wa Marekani, kwa maoni yangu tungekuwa katika vita vikubwa na Korea kaskazini hivi sasa.

“Bado kazi kubwa imesalia, lakini uhusiano wangu na Kim Jong-un ni mzuri.”

Amesema nini kuhusu umoja wa kisiasa?

Baada ya miaka miwili ya ufuasi wenye uhasama, Trump ameregelea wito wa umoja wa kisiasa ambao ameutoa katika hotuba zake mbili zilizopita za kila mwaka bungeni.

“Pamoja tunaweza kuvunja mkwamo wa kisiasa wa miongo kadhaa,” amesema.

“Tunaweza kuziba migawanyiko ya siku za nyuma, tukaponya vidonda vya jadi, na kujenga muungano mpya.”

Trump ameelezea maeneo ambayo yanaweza kufikiwa makubaliano, kama kuimarisha miundo mbinu, kupunguza bei za dawa na kupambana na saratani kwa watoto.

Lakini saa chache kabla ya hotuba hiyo, Chuck Schumer, kiongozi wa Seneti wa chama cha Democratic amemshutumu Trump kwa “kuidhinisha taifa lenye mgawanyiko” kwa sehemu kubwa ya mwaka.

Katika chakula cha mchana na waandishi habari kwenye ikulu ya White House Jumanne, Trump alimuita Schumer “muovu”, na kutumia tusi, New York Times inaripoti.

Wakati Trump akitoa hotuba yake kwa taifa Jumanne usiku, mpinzani wake mkuu alikuwa amekaa nyuma yake.

Kiongozi wa Democrats katika bunge la wawakilishi, Spika Nancy Pelosi, aliidhinisha upinzani kwa matakwa ya rais kuhusu ufadhili wa ujenzi wa ukutana mara nyingi humkebehi.

Democrats wamejibu nini?

Stacey Abrams, aliyepoteza kiti chake kuwania Ugavana wa jimbo la Georgia, aliwasilisha ujumbe wa Democrats kwa Trump.

Alikuwa mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi aliyejibu kwa upinzani mkali.

Bi Abrams amesema: ” hatua ya serikali kusitisha ufadhili ni njama iliyopangwa na rais, na ambayo imekiuka kila ncha ya usawa na ambayo sio tu ambayo haikuwajali raia – lakini pia maadili.”

Wakati wa hotuba ya Trump wabunge kadhaa wanawake wa Democratic walivaa nguo nyeupe, rangi iliyoidhinishwa na kundi la wanawake katika karne ya 20 waliokuwa wakidai haki ya kupiga kura.

Walikaa kimya pasi kucheka wakati wenzao wa Republican walipoinuka wakipiga makofi kushangilia aliyoyasema rais.

Lakini wanachama wa Democrats walimshangaza Trump kwa kumsimamia kwaheshima kiongozi huyo aliposema kwamba kuna wanawake zaidi wanofanya kazi bungeni, kuliko ilivyowahi kushuhudiwa katika siku za nyuma.

“Vizuri sana!” alisema rais baada ya muitikio huo. “Vizuri sana”

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *