Trump atishia kuuangamiza uchumi wa Uturuki kuhusu Wakurdi Syria

Trump atishia kuuangamiza uchumi wa Uturuki kuhusu Wakurdi Syria

Like
670
0
Monday, 14 January 2019
Global News

Rais wa Marekani Donald Trump ametishia ‘kuiangamiza Uturuki kiuchumi’ iwapo taifa hilo litawashambuliwa vikosi vya wakurdi nchini Syria baada ya wanajeshi wa Marekani kuondoka Syria.

Katika ujumbe wake alioutuma kwenye mtandaoi wa kijamii Twitter, Trump amesema hakutaka Wakurdi kwa upande wao nao pia waichokoza Uturuki.

Vikosi vya Marekani vimepambana kwa ushirikiano na wanamgambo wa Kikurdi kaskazini mwa Syria dhidi ya kundi la Islamic State (IS).

Uturuki hatahivyo inatazama wapiganaji hao wa vitengo vya YPG kama magaidi.

Rais Recep Tayyip Erdogan amezungumza kwa hasira kuhusu Marekani kuliunga mkono kundi hilo, na kuapa kuliangamiza.

Kauli ya Trump Jumapili inafuata shutumza zaidi dhidi ya uamuzi wake wa ghafla kuondosha vikosi vya Marekani kutoka Syria.

Afisa mkuu kutoka familia ya kifalme Saudia, Prince Turki al-Faisal, ameiambia BBC kwamba itakuwa na ‘athari mbaya’ ambayo huenda Iran, rais wa Syria Bashar al Assad na Urusi zikafaida kutokana kwayo.

Waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo kwa sasa yuko katika mji mkuu wa Saudia Riyadh anapozuru Mashariki ya kati kuwahakikishia washirika wa Marekani katika eneo.

Trump amesema nini?

Rais ametetea uamuzi wake kuondoa vikosi, akieleza kuwa wapiganaji wowote waliosalia wa IS wanaweza kushambuliwa kutoka eneo ambalo halikutajwa, ‘lililopo katika kambi za karibu’.

Hakueleza namna uchumi wa Uturuki utakavyoathirika iwapo taifa hilo litawashambulia wapiganaji wa YPG. Trump pia ametaja kuundwa kwa ‘eneo salama la maili 20’ ambalo mwandishi wa BBC Barbara Plett Usher anasema linadokezea aina ya suluhu ambayo Pompeo anajaribu kuijadili.

Rais pia alisema Urusi, Iran na Syria ndio wafaidi wakuu wa hatua ya Marekani Syria na kwamba wakati umefika kuwarudisha nyumbani wanajeshi wa Marekani.

Msemaji wa rais Erdogan Ibrahim Kalin amejibu katika ujumbe wa Twitter akisema Uturuki ilitarajia Marekani ‘kuheshimu ushirikiano wetu wa kimipango’.

“Magaidi hawawezi kuwa washirika na wandani wako,” alisema.

Trump aliwashangaza washirika na kukabiliwa na shutuma kali nyumbani mwezi uliopita walipoagiza vikosi vya Marekani kuondoka mara moja kutoka 30% ya maeneo yanayodhibitiwa na muungano wa vikosi Syria (SDF) unaoongozwa na YPG nchini Syria.

Mike Pompeo amesema nini?

Mwishoni mwa juma, Pompeo amesema amezungumza na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu kwa simu na ana matumaini kwamba makubaliano yatafikiwa na Uturuki kuwalinda wapiganaji wa Kikurdi. Hakutoa maelezo zaidi.

Akizungumza huko Abu Dhabi, Pompeo amesema Marekani inatambua “haki ya watu wa Uturuki na haki ya Rais Erdogan kuilinda nchi yake dhidi ya magaidi”.

“Tunafahamu pia kuwa wanaopigana kwa ushirikiano wetu kwa wakati huu wote wana haki ya kulindwa pia, “aliongeza.

Huko Riyadh, Waziri huyo wa mambo ya nje anatarajiwa kuijadili Iran na mizozo nchini Yemen na Syria, Vyombo vya habari Marekani vinaripoti, pamoja na kutafuta taarifa zaidi kuhusu uchunguzi wa mauaji ya mwandishi mashuhuri Jamal Khashoggi.

Khashoggi, mkosoaji mkuu wa utawala wa Saudi Arabia aliuawa katika ubalozi wa Saudia mjini Istanbul miezi mitatu iliyopita.

Kuna wanajeshi wangapi Syria?

Takriban maafisa 2,000 wa jeshi la Marekani inaarifiwa wapo kaskazini mwa Syria.

Wanajeshi wa nchi kavu waliwasili mnamo 2015 wakati rais Barack Obama alipotuma idadi ndogo ya vikosi maalum kutoa mafunzo na ushauri kwa wapiganaji wa YPG.

Marekani ilifanya hivi baada ya jitihada kadhaa kujaribu kuwafunza na kuyahami makundi ya waasi Syria kupambana na wapiganaji, kuishia kwa vita.

Katika miaka iliyofuata idadi ya wanajeshi wa Marekani iliongezeka Syria, na kukaidhinishwa kambi na vituo vya kutua ndege za kijeshi katika eneo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *