Trump ayataka mataifa ya NATO kuongeza bajeti ya ulinzi

Trump ayataka mataifa ya NATO kuongeza bajeti ya ulinzi

Like
624
0
Thursday, 12 July 2018
Global News

Katika hatua nyingine Trump ameilaumu Ujerumani kwa madai kwamba inatumia kiasi kidogo, katika bajeti ya ulinzi wakati ambapo inatumia fedha nyingi katika ununuzi wa bidhaa za nishati, kutoka nchini Urusi,taifa ambalo walipa kodi wa Marekani wanachangia kodi zao kukabiliana na vitisho vyake.

Kansela wa Ujeruman Bi Angela Merkel,amejibu shutuma hizo za Trump na kudai idadikubwa ya wanajeshi wake wapo katika vikosi vya NATO

Bi Merkel Anasema “sisi ni taifa la pili kuwa na kikosi kikubwa cha wanajeshi wetu,tunanatoa mchango mkubwa kijeshi kwa NATO na kushiriki kwa kiwango kikubwa kule Afghanistan,kulinda hata maslahi ya Marekani kwa sababu ya ushiriki wao Afghanstan,jambo ambalo ni mfano wa kuiunga mkono Marekani, kwa mjibu wa kifungu namba tano cha NATO” Bi Merkel.

Hata hivyo katika mkutano wao wa pamoja na waandishi wa Habari na Bi Angela Merkel,Trump ameonekana kubadili msimamo wake na kuwa na kauli za kuiunga mkono Ujerumani.

“Tumekuwa na mkutano mzuri,tunajadili matumizi ya kijeshi,tunazungumza kuhusiana na biashara.Tuna uhusiano mzuri sana na Kansela na uhusiano mzuri na Ujerumani. Tunaamini kuwa tunafikia mafanikio makubwa sana,na biashara yetu itakua,na mambo mengine mengi yataongezeka.Lakini tunasubiria na kuona nini kinatokea miezi michache ijayo”.

Mkutano wa Brussels unakuja ikiwa ni takribani wiki moja tu kabla ya Rais Trump kuwa na mkutano wa kwanza na rais wa Urusi Vladmir Putin mjini mjini Helsinki nchini Finland.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *