SAUTI: TUME YA KUDHIBITI DAWA ZA KULEVYA YATOA TAKWIMU

SAUTI: TUME YA KUDHIBITI DAWA ZA KULEVYA YATOA TAKWIMU

Like
276
0
Tuesday, 16 December 2014
Local News

IMEELEZWA KUWA zaidi ya gramu elfu 3 za dawa za kulevya kutoka viwandani zimekamatwa katika kipindi cha kuanzia mwezi juni hadi Novemba mwaka huu zikihusisha watuhumiwa 24 ambapo kati ya hao watuhumiwa 7 ni raia wa Tanzania na 17 ni raia wa kigeni.

Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkemia kutoka Tume ya kudhibiti dawa za kulevya nchini ALOYCE NGONYANI wakati akizungumza na Efm juu ya mikakati ya kuzuia uingizwaji wa dawa hizo hususani kipindi hiki cha mwisho wa mwaka.

NGONYANI amesema kuwa ingawa kumekuwa na ongezeko kubwa la uingizwaji wa dawa hizo lakini wameandaa mikakati madhubuti ya kupambana na tatizo hilo kupitia kikosi maalumu cha Taifa cha kupambana na dawa hizo ikiwemo kuwashirikisha zaidi wananchi ili kupunguza athari zinazojitokeza kutokana na matumizi ya dawa hizo kwa jamii.

Mbali na hayo ameeleza kuwa katika utendaji wao wa kazi wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo wahusika kutumia mbinu tofauti katika kuingiza dawa hizo nchini.

 

 

Comments are closed.