TUME YA TAIFA ya Uchaguzi imetangaza Matokeo ya Zoezi la Uandikishaji wa Wapigakura katika Daftari la Kudumu kwa mfumo wa BIOMETRIC VOTERS REGISTRATION-BVR katika majimbo matatu ya Bunju,Katavi na Kilombelo ambapo zoezi limeonyesha Mafanikio makubwa.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji DAMIAN LUBUVA amesema zoezi hilo limefanikiwa kufikia malengo ambapo katika jimbo la Bunju wameandikishwa watu 21,323 kati ya 35,486, Jimbo la Katavi ni 11,210 kati ya 11394 na Kilombero ni 19188.