AWAMU ya pili ya Uchaguzi wa rais nchini Tunisia inatarajia kufanyika siku ya Jumapili.
Taarifa zaidi zimeeleza kuwa Rais aliyeko madarakani, MONCEF MARZOUKI atapambana na mkongwe wa siasa, BEJI CAID ESSEBSI.
Kwa mara ya kwanza Watunisia wataruhusiwa kumchagua Rais wao kwa uwazi tangu nchi hiyo ilipopata Uhuru wake kutoka kwa Ufaransa, mwaka 1956.
Awamu ya kwanza ya uchaguzi wa Rais imefanyika Novemba 23, na Bwana ESSEBSI, mwenye umri wa miaka 88, amepata asilimia 39 ya kura, kiwango ambacho hakikutosha kumpa ushindi wa moja kwa moja.