TURNBULL AAPISHWA KUWA WAZIRI MKUU MPYA AUSTRALIA

TURNBULL AAPISHWA KUWA WAZIRI MKUU MPYA AUSTRALIA

Like
221
0
Tuesday, 15 September 2015
Global News

MALCOLM Turnbull ameapishwa kuwa waziri mkuu mpya wa Australia baada ya kuondolewa katika mamlaka kwa aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Tony Abbott.

Turnbull aliyekuwa waziri wa mawasiliano katika serikali ya Abbott, sasa atakuwa waziri mkuu wa nne nchini humo tangu 2013 ambaye amesema kuwa huo ndio wakati bora zaidi wa kuwa raia wa Australia.

Abbott, aliyeondolewa mamlakani Jumatatu baada ya kura ya haraka kufanywa katika chama tawala cha Liberal, amesema aliondolewa kwa “uchungu” lakini ameahidi kurahisisha shughuli ya mpito kadiri anavyoweza.

Comments are closed.