TUTAPAMBANA YAPOKEA MILIONI 5 KUENDELEZA KIKUNDI HICHO

TUTAPAMBANA YAPOKEA MILIONI 5 KUENDELEZA KIKUNDI HICHO

Like
297
0
Wednesday, 19 November 2014
Local News

JUMLA ya shilingi milioni tano zimetolewa na Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini Mh Abdul Azizi Mohamed Abood katika kikundi cha kuweka na kukopa cha Tutapambana Silk kilichopo Chamwino Mjini Morogoro kwa ajili ya kuendeleza kikundi hicho katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akipokea msaada huo Katibu wa kikundi hicho Omary Simbeye amesema kuwa fedha hizo zitawasaidia kuweza kuiendeleza miradi hiyo ikiwa ni pamoja na kujenga ofisi na kukabiliana na changamoto mbalimbali za ukosefu wa ofisi katika kikundi hicho.

Aidha amesema kuwa kikundi hicho ambacho kina undwa na wanaume pekee mpaka sasa kikiwa na miradi mbalimali ikiwemo mradi wa kuku, duka na mikopo ya riba ambayo inawawezesha wanachama hao kuweza kujikwamua kiuchumi.

Comments are closed.