TUZO ZA OSCAR: BAADA YA KULAUMIWA SANA WAANDAJI WAJA NA MAAMUZI HAYA

TUZO ZA OSCAR: BAADA YA KULAUMIWA SANA WAANDAJI WAJA NA MAAMUZI HAYA

Like
335
0
Thursday, 30 June 2016
Entertanment

Waandalizi wa tuzo za Oscar wametangaza kuwa wamewaalika wanachama wapya zaidi kupiga kura ya maamuzi ya washindi wa mwaka huu, baada ya malalamishi makubwa ya mwaka uliopita ambapo walilaumiwa kwa kuyabagua makundi mengine ya watu.

Waandalizi hao wa The Academy of Motion Picture Arts and Sciences wanasema wamewaalika karibu watu 700, wakiwalenga hasa wanawake na watu kutoka jamii za watu wachache.

Miongoni mwa wale ambao wamealikwa kushiriki katika uteuzi wa washindi wa tuzo hizo ni wacheza filamu weusi, na vilevile waigizaji weusi kutoka Uingereza Idris Elba na John Boyega.

Wachezaji filamu kadhaa wa Hollywood walisusia sherehe za tuzo hizo mnamo mwezi Februari kwa sababu walioteuliwa katika tuzo hizo, hakuwemo mtu kutoka jamii za watu wachache.

Comments are closed.