TWAWEZA KUFANYA MDAHALO WA WAGOMBEA URAIS OCTOBER 18

TWAWEZA KUFANYA MDAHALO WA WAGOMBEA URAIS OCTOBER 18

Like
258
0
Friday, 16 October 2015
Local News

TAASISI isiyokuwa ya Kiserikali ya Twaweza inatarajia kuandaa mdahalo wa wagombea urais unaotarajiwa kufanyika tarehe 18 0ktoba mwaka huu kwa lengo la kuwawezesha Wagombea waweze kutoa sera zao kwa Wananchi  pamoja na kuruhusu Wananchi hao kuwauliza maswali Wagombea wao ili waweze kufanya maamuzi sahihi siku ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 Mwaka huu.

 

Mkurugenzi wa Twaweza Aidan Eyakuze amesema kuwa hadi sasa wamepata uthibitisho wa ushiriki wa vyama vine vya siasa ambavyo  ni ACT- Wazalendo , Alliance for Democratic Change ADC, Chama cha Mapinduzi CCM na Chama cha Ukombozi wa Umma CHAUMA na kuwa bado wanawasiliana na uongozi wa CHADEMA.

Comments are closed.