KATIKA kuhakikisha jitihada za kuboresha Sekta ya elimu nchini zinaleta mafanikio, asasi ya utafiti ya -TWAWEZA-kupitia mradi wake wa uwezo imeendesha mafunzo ya siku mbili katika wilaya ya mwanga yenye lengo la kuwapa ujuzi wa kufanya kazi za kujitolea vijana wapatao 60 ili waweze kufanya tathmini juu kwa watoto katika nyanja za kuhesabu pamoja na kusoma kiswahili na kingereza.
Akizungumza na E-FM Mratibu wa Mradi huo George Madundo amesema mafunzo hayo yatachangia katika shughuli za ukusanyaji wa taarifa za kubaini hali halisi ya uelimishaji wa watoto walio kati ya umri wa miaka 7 hadi 16 wilayani hapo.
Naye katibu tawala wilaya ya mwanga Yusufu Kasuku ameeleza kuwa kutokana na mradi wa uwezo wataweza kupata watalamu wengi watakaoweza kufanya tathmini ya mwelekeo mzima wa elimu.