Uchaguzi DRC: Felix Tshisekedi asema hamuungi mkono mgombea wa upinzani

Uchaguzi DRC: Felix Tshisekedi asema hamuungi mkono mgombea wa upinzani

Like
503
0
Tuesday, 13 November 2018
Global News

Felix Tshisekedi kiongozi wa chama kikubwa zaidi cha kisiasa nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, ameondoa uungwaji mkono wake wa kuwa na mgombea mmoja wa upinzani kwa uchaguzi ambao utafanyaika Disemba 23.

Kiongozi huyo wa chama cha Union for Democracy and Social Progress alitoa tangazo hilo siku moja bada ya makuabaliano hayo kutangazwa.

“Ninasema kuwa makubaliano yaliyoafikiwa Geneva hayajakubaliwa mashinani na yalikataliwa nao. Kutokana na hilo, ninaondoa uungwaji mkono wangu kutoka kwa makubaliano hayo, tuliyoyasaini jana,” Bw Tshisekedi alisema wakati wa mahojiano na kituo cha radio cha Top Congo.

Viongozi saba wa upinzani, wanaokutana huko Uswizi siku ya Jumapili, walimchagua mbunge asiye na umaarufu Martin Fayulu kuwa mgombea wao.

Rais Joseph Kabila ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 18, atang’atuka bada ya uchaguzi uliosubiriwa kwa muda mrefu.

Kiongozi mwingine wa upinzani Vital Kamerhe pia alijitoa kwenye makubaliano hayo akisema hakukuwa na uungwaji mkono wa kutosha kutoka mashinani baina ya wanachama.

Chama tawala kimemchagua Emmanuel Ramazani Shadary, mtiifu kwa Rais Joseph Kabila kuwa mgombea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *