UCHAGUZI KINONDONI MISINGI YA DEMOKRASIA ILIKIUKWA

UCHAGUZI KINONDONI MISINGI YA DEMOKRASIA ILIKIUKWA

Like
293
0
Tuesday, 03 November 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa uchaguzi wa wabunge na madiwani katika jimbo la kinondoni  uliofanyika oktoba 25 mwaka huu haukuzingatia baadhi ya misingi ya haki inayoongozwa na demokrasia ya kweli kutokana baadhi ya wagombea wa vyama mbalimbali vya siasa kutoshirikishwa katika hatua zote.

 

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Katibu mwenezi wa Taifa wa chama cha Sauti ya Umma-SAU-ambaye pia alikuwa mgombea wa nafasi ya ubunge jimboni hapo kupitia chama hicho Johnson Mwangosi wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mchakato wa zoezi hilo katika Jimbo hilo.

 

Amebainisha kuwa mbali na wabunge kutoshirikishwa pia mawakala wa vyama walifukuzwa katika ukumbi ambao ulikuwa unatumika kujumuisha kura zote zilizopigwa na wananchi kwa ngazi zote za uongozi.

Comments are closed.