UCHAGUZI WAANZA AFRIKA YA KATI

UCHAGUZI WAANZA AFRIKA YA KATI

Like
220
0
Wednesday, 30 December 2015
Global News

WANANCHI wa  Jamuhuri ya Afrika ya kati hii leo wanashiriki katika zoezi la uchaguzi wa Rais na wabunge  nchini humo.

 

Uchaguzi huo uliokuwa ufanyike tarehe 27 mwezi huu ulisogezwa mbele na tume ya uchaguzi nchini humo hadi  tarehe ya leo Desemba 30 kutokana na kasoro zilizojitokeza wakati wa kipindi cha maandalizi ya uchaguzi huo.

 

Msemaji wa Tume ya uchaguzi nchini humo Julius Rufin Ngoadebaba ameahidi kuwa uchaguzi huo utakwenda vizuri katika maeneo yote nchini humo  ambako Zaidi ya watu milioni 1.8 wanatarajia kupiga kura katika vituo zaidi ya 500 vilivyoandaliwa kwa ajili  ya zoezi hilo.

Comments are closed.