UCHUMI UKIRUHUSU TUTAFUNGUA BALOZI KATIKA MATAIFA MENGINE

UCHUMI UKIRUHUSU TUTAFUNGUA BALOZI KATIKA MATAIFA MENGINE

Like
269
0
Thursday, 05 February 2015
Local News

 

TANZANIA imesema kuwa dhamira yake ya kufungua balozi katika baadhi ya nchi duniani iko pale pale na itatekeleza mpango wake huo kwa kadri hali ya fedha na uchumi inavyoruhusu.

Aidha, Tanzania imesema kuwa itaendelea kushirikiana na Iran katika kupambana na kukabiliana na ugaidi duniani kwa sababu nchi mbili hizo, kama ilivyo dunia nzima, zinahitaji dunia tulivu na inayosaka maendeleo ya watu bila usumbufu na vitisho vya ugaidi.

Mambo hayo mawili yamejadiliwa katika mazungumzo kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran, Mheshimiwa Javad Zarif.

Mheshimiwa Zarif amewasili nchini jana akitokea Burundi katika ziara ambayo pia imemfikisha Kenya, Uganda na Rwanda akifuatana na maofisa wa Serikali na kundi kubwa la wafanyabiashara wa Iran.

iran4

Comments are closed.