UDOM YAANDAA HAFLA KUMUENZI RAIS KIKWETE

UDOM YAANDAA HAFLA KUMUENZI RAIS KIKWETE

Like
197
0
Tuesday, 25 August 2015
Local News

CHUO kikuu cha Dodoma-UDOM-kinatarajia kufanya hafla ya kumuenzi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dokta Jakaya Mrisho Kikwete kama sehemu ya kutambua mchango wake wa kuwezesha kujengwa kwa chuo hicho.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa chuo hicho profesa Idris Kikula wakati akizungumza na baadhi ya mabalozi na maafisa wa uwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania katika umoja wa mataifa inasema kuwa Rais Kikwete amefanya kazi kubwa katika kuhimiza na kufanikisha ujenzi wa chuo hicho.

Profesa Kikula na ujumbe wake yupo ziarani nchini Marekani, ziara iliyofikisha Jijini New York na kupata nafasi ya kukagua vifaa tiba na vitabu mbalimbali vya kiada vilivyotolewa kwa serikali ya Tanzania.

Comments are closed.