UEFA: WABABE WA JIJI LA MADRID WATOANA JASHO

UEFA: WABABE WA JIJI LA MADRID WATOANA JASHO

Like
675
0
Wednesday, 15 April 2015
Slider

Wababe wa jiji la Madrid nchini Hispania jana wameshindwa kutambina katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Mabingwa barani Ulaya,UEFA, hatua ya robo fainali baada ya kutoka sare ya bila kufungana 0-0.

Katika mchezo huo uliochezwa katika dimba la Vicente Calderon Athletico Madrid walikuwa wenyeji wa Real Madrid ambapo timu hizo zitarudiana katika uwanja wa Bernabeu tarehe 22 Aprili.

Nyota ya mshambuliaji wa real Madrid Gareth Bale ilishindwa kung’aa jana baada ya kukosa nafasi ya wazi mnamo dakika ya tatu ya mchezo katika kipindi cha kwanza nah ii imetokana na kipa wa Atletico Madrid Jan Oblak kuutumia vyema mchezo huo wa jana kwa kuhakikisha anapangua michomo ya washambuliaji wa Real madrid

M2

 

Mchezo mwingine uliochezwa jana usiku ulizikutanisha Juventus ya Italia na Monaco ya Ufaransa. Matokeo ni kwamba Juventus imeibuka na ushindi wa goli 1-0. Juventus ilipata bao lake pekee katika dakika ya 57 kwa njia ya penalti ikifungwa na Vidal. Juventus inalenga pia kufika hatua ya nusu fainali ambapo kwa mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2003. Hata hivyo kocha wa Monaco Leonardo Jardim, ameilalamikia penalti hiyo kuwa haikuwa ya haki. Timu hizi nazo zitarudiana huko Monaco Aprili 22.

Michezo mingine miwili ngazi ya robo fainali itakayopigwa Jumatano itazipambanisha FC Porto ya Ureno dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani, huku Paris Saint Germain ya Ufaransa ikiikaribisha Barcelona ya Hispania.

J J2

Comments are closed.