MAAFISA kutoka Ufaransa na Uingereza wamesaini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa usalama katika kivuko kimoja muhimu cha mpakani, huku wakitangaza hatua zikiwemo teknolojia ya kisasa ili kuwadhibiti wahamiaji na waomba hifadhi wanaojaribu kuingia Uingereza.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Bernard Cazeneuve na mwenzake wa Uingereza Theresa May, wamesaini makubaliano ya muafaka jana katika mji wa bandari wa Calais, ambako mamia ya watu wamejaribu kuvuka mpaka na kuingia Uingereza kutokea Ulaya katika kipindi cha mwaka huu ulioshuhudia ongezeko la shinikizo la wahamiaji.