UFARANSA: NATIONAL FRONT PARTY YAONGOZA MATOKEO YA AWALI

UFARANSA: NATIONAL FRONT PARTY YAONGOZA MATOKEO YA AWALI

Like
246
0
Monday, 07 December 2015
Global News

KURA zilizohesabiwa katika awamu ya kwanza ya uchaguzi wa kikanda nchini Ufaransa, zinaonyesha chama cha National Front Party kinaongoza katika matokeo kwa asilimia 30 ya kura zote zilizopigwa.

Uchaguzi huo ni wa kwanza kufanyika tangu kundi la kigaidi la wanamgambo wa dola ya Kiislamu la Islamic State kuua watu 130 mjini Paris mwezi uliopita.

Chama Tawala cha kisoshalisti kimeshika nafasi ya tatu katika kura ingawa kimelazimika kujiondoa katika uchaguzi wa awamu ya pili katika mikoa miwili ikiwa ni jitihada za kukizuia chama cha National Front kuchukua ushindi maeneo hayo.

 

Comments are closed.