UFARANSA imeanzisha mashambulizi mapya ya anga usiku wa kuamkia leo nchini Syria dhidi ya kambi ya mafunzo ya kundi la Dola la Kiislamu-IS na mashambulizi zaidi yatafuata.
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, amesema leo kuwa nchi hiyo imewashambulia wapiganaji hao, na haitakuwa mara ya mwisho.
Wakati huo huo, taarifa zinaeleza kuwa mshauri wa kijeshi wa Iran, Jenerali Hussein Hamdani, ameuawa na wanamgambo wa IS nchini Syria.