UFARANSA YACHUNGUZA MABAKI YA NDEGE YANAYOSADIKIWA KUWA NI NDEGE YA MALAYSIA MH370

UFARANSA YACHUNGUZA MABAKI YA NDEGE YANAYOSADIKIWA KUWA NI NDEGE YA MALAYSIA MH370

Like
204
0
Thursday, 30 July 2015
Global News

MAMLAKA ya usafirishaji nchini Ufaransa imesema inachunguza mabaki ya ndege ya yanayodaiwa kupatikana ndani ya Bahari ya Hindi ili kubaini kama ni ya ndege ya Malaysia ya MH370 iliyopotea bila kuwa na taarifa zozote kwa muda mrefu sasa.

Taarifa kutoka Marekani zinasema wachunguzi hao ambao wameona picha za mabaki hayo wana uhakika mkubwa kwamba ni ya ndege hiyo ya Malaysia ambapo mabaki hayo ni sehemu ya bawa la ndege.

Hata hivyo, Wataalamu wa Ufaransa wanasema ni mapema mno kutoa uhakika kwamba mabaki hayo ni lazima yatakuwa ya ndege ya Malaysia aina ya Boeing 777 ambayo kupotea kwake kumeleta gumzo la kidunia.

Watu wapatao 239 waliokuwa wakisafiri na ndege hiyo walipoteza maisha.

Comments are closed.