UFARANSA YAPENDEKEZA HATUA KALI KUSITISHA MAUAJI BURUNDI

UFARANSA YAPENDEKEZA HATUA KALI KUSITISHA MAUAJI BURUNDI

Like
275
0
Tuesday, 10 November 2015
Global News

UFARANSA imependekeza hatua kali zichukuliwe kwaajili ya kusitisha mauaji ambayo yamekuwa yakiendelea nchini Burundi.

Taifa hilo liliwasilisha muswada wa mapendekezo kwa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatatu iliyopita likieleza wasiwasi wake juu ya hali ya usalama nchini Burundi.

Ghasia zilianza mwezi Aprili baada ya maandamano ya kupinga hatua ya Rais Pierre Nkurunziza kutangaza kuwania urais kwa muhula wa tatu huku ikiaminika kuwa Machafuko hayo ndiyo mabaya zaidi nchini humo katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Comments are closed.