UFARANSA YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA BRAZIL

UFARANSA YASHINDWA KUTAMBA MBELE YA BRAZIL

Like
448
0
Friday, 27 March 2015
Slider

Richa ya timu ya taifa ya Ufaransa kuanza kuliona lango la Brazil katika dakika ya 21 kwa goli lililofungwa na Raphael Varane, kikosi cha Brazil kilijipanga vyema kuhakikisha wanaondoka na ushindi katika mchezo huo.

Bao la kusawazisha la Brazil lilifungwa na Oscar dos Santos Emboaba Júnior katika dakika ya 40 kasi iliongezeka kwa kuindama safu ya ulinzi ya Ufaransa na hatimaye wakaongeza  magoli mengine mawili kupitia kwa Neymar da Silva Santos, Júnior, na Luiz Gustavo na hivyo hadi mechi hiyo inamalizika Brazil 3 Ufaransa 1.

B4

B3

Katika mechi nyingine za kimataifa za kirafiki zilizochezwa hapo jana, Bahrain iligeuzuwa chapati na Colombia pale waliposhindiliwa magoli 6 kwa mtungi huku Iran ikiwapa darasa Chile kwa kuichabanga magoli mawili kwa nunge.

Leo kutakuwa na mechi moja ya kimataifa ya kirafiki ambapo Canada watairibisha Guatemala

Comments are closed.