UFARANSA YAZUIA SHAMBULIO LA KIGAIDI

UFARANSA YAZUIA SHAMBULIO LA KIGAIDI

Like
161
0
Thursday, 16 July 2015
Global News

WAZIRI wa Mambo ya ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve amesema vyombo vya usalama nchini humo vimefanikiwa kuwakamata watu wanne wanaodaiwa kupanga njama za kushambulia maeneo ya jeshi.

Bernard amesema kuwa watu hao wanaoshikiliwa miongoni mwao yupo mmoja aliwahi kuwa mwanajeshi mwenye umri wa miaka 30.

Idara za usalama nchini Ufaransa kwa sasa zimekuwa makini zaidi tangu kufanyika kwa mashambulizi yaliyosababisha mauaji ya watu yanayodaiwa kutekelezwa na kundi la wapiganaji wa Kiislam.

Comments are closed.