UFINYU WA WODI WAWALAZA KITANDA KIMOJA WAZAZI NA WATOTO

UFINYU WA WODI WAWALAZA KITANDA KIMOJA WAZAZI NA WATOTO

Like
271
0
Monday, 28 December 2015
Local News

AKINAMAMA wajawazito na watoto   katika hospitali ya wilaya ya maswa  Mkoani Simiyu, wamekuwa wakilazimika kulala kitanda kimoja watu wawili na muda mwingine kupeana zamu kutokana na ufinyu wa wodi, na upungufu wa vitanda   suala ambalo linaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa.

 

Kufuatia hali hiyo, wakizungumza na Efm wameiomba  serikali kuyafungua majengo  mapya  ambayo tayari yameshakamilika ili kuweza kupunguza adha hiyo.

 

Kituo hiki kimeshuhudia akinamama hao wakiwa wamelala wawili wawili wodini, huku baadhi wakiwa wamejifungua watoto na wengine kushindwa kulala kutokana na upungufu   wa vitanda .

Comments are closed.