UFISADI: WAZIRI WA UCHUMI JAPAN AJIUZULU

UFISADI: WAZIRI WA UCHUMI JAPAN AJIUZULU

Like
197
0
Thursday, 28 January 2016
Global News

WAZIRI wa uchumi nchini Japan Akira Amari amejiuzulu kutokana na madai ya ufisadi yaliyokuwa yakimkabili.

Bwana Amari ametoa tangazo hilo ghafla katika mkutano na waandishi wa habari jana ambapo mbali na hayo amekanusha kupokea hongo kutoka kwa kampuni moja ya ujenzi kama ilivyodaiwa na jarida moja la Japan.

Hatua hiyo imechukuliwa kama pigo kubwa kwa waziri mkuu Shinzo Abe kwani Amari alitarajiwa kusafiri hadi New Zealand wiki ijayo kusaini mkataba wa ushirikiano kati ya mataifa ya ng’ambo ya pili ya bahari ya Pacific.

Comments are closed.