POLISI nchini Senegal wamewakamata watu wapatao mia tisa katika kamata kamata ya watu wanaoshukiwa kujihusisha na ugaidi.
Zoezi hilo limefanyika mwishoni mwa juma lililopita katika mji mkuu wa Dakar karibu na mtaa wa Thies huku Jeshi la ulinzi likitoa angalizo tangu shambulio lililowahi kutokea mapema mwezi huu katika hoteli iliyoko mji mkuu wa Burkina Faso.
Hata hivyo wiki iliyopita waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Abdoulaye Daouda Diallo amezitaka hoteli zote nchini humo kuongeza ulinzi ili kuzuia matukio kama hayo.