UGAIDI: RAIA WA UINGEREZA AHUKUMIWA KENYA

UGAIDI: RAIA WA UINGEREZA AHUKUMIWA KENYA

Like
201
0
Wednesday, 02 December 2015
Global News

MTU mmoja raia wa Uingereza, anayetuhumiwa kupanga mashambulio ya kigaidi, amefungwa jela miaka tisa na mahakama mjini Mombasa nchini Kenya.

Jermaine Grant Mwingereza aliyekamatwa mwaka 2011, amefungwa jela kwa makosa tisa yanayohusiana na kujaribu kujipatia uraia wa Kenya kwa njia haramu.

Bado anakabiliwa na mashtaka ya “kupanga kuunda vilipuzi” kwenye kesi ambayo bado inaendelea mjini Mombasa lakini Grant amekanusha mashtaka hayo.

 

Comments are closed.