UGAIDI: WATOTO MILIONI MOJA WAACHA MASOMO

UGAIDI: WATOTO MILIONI MOJA WAACHA MASOMO

Like
200
0
Tuesday, 22 December 2015
Global News

SHIRIKA la umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto-UNICEF- limesema kuwa mashambulizi kutoka kwa wanamgambo wa Boko Haram nchini Nigeria na kwenye nchi zingine yamesababisha zaidi ya watoto milioni moja kuacha masomo.

Katika ripoti mpya, iliyotolewa na shirika hilo imeeleza kuwa mamia ya shule nchini humo zimeshambuliwa, kuporwa na kuchomwa moto wakati wa mzozo huo ambao umedumu kwa kipindi cha miaka sita.

Licha ya Amri ya rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari kwa makamanda wake wa jeshi kuzuia mashambulizi ya Boko Haram, bado kundi hilo linaendelea kuwaua watu katika ukanda wa Magharibi mwa Afrika.

Comments are closed.