UGIRIKI WAPIGA KURA YA HAPANA

UGIRIKI WAPIGA KURA YA HAPANA

Like
190
0
Monday, 06 July 2015
Global News

MAELFU ya raia wa Ugirik usiku wa kuamkia leo wametawanyika katika mitaa ya mjini Anthens karibu na jengo la bunge, wakifurahia kura ya hapana waliyoipiga ambayo imeshinda kwa ya asilimia 60.

Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras,amesema matokeo hayo ya hapana, hayana nia ya kwenda kinyume na jumuiya ya Ulaya bali yataiongezea Ugiriki uwezo wa majadiliano zaidi kuhusiana na mzozo wa madeni.

Tsipras ameongeza kuwa serikali ya Ugiriki iliitisha kura hiyo ya maoni ikiamini kuwa kura ya Hapana italeta makubaliano mazuri, pamoja na kwamba kuna onyo kutoka kwa viongozi wa ukanda wa Euro kuwa hatua hiyo itasababisha Ugiriki kuondolewa katika nchi wananchama wa ukanda huo.

Comments are closed.