UGUMU WA MAISHA WATAJWA KUWA CHANZO CHA KUPOROMOKA KWA MAADILI

UGUMU WA MAISHA WATAJWA KUWA CHANZO CHA KUPOROMOKA KWA MAADILI

Like
552
0
Friday, 27 March 2015
Local News
UGUMU wa maisha nchini umetajwa kuwa ni miongoni mwa  chanzo cha kuporomoka kwa maadili katika jamii.
Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wamedai kuwa hali ngumu ya kimaisha inasababisha wazazi kuishi chumba kimoja na watoto hali inayopelekea watoto hao kuiga baadhi ya vitu wanavyoviona kwa wazazi muda ambao wazazi wanadhani watoto hao wamelala.
Wameongeza kuwa kumekuwa na matukio mbalimbali ya watoto kubakana wenyewe kwa wenyewe na hata baadhi ya watoto wa kiume kuingiliwa kinyume cha maumbile.
 

Comments are closed.