UHUSIANO WA ZIKA NA VICHWA VIDOGO WATHIBITISHWA

UHUSIANO WA ZIKA NA VICHWA VIDOGO WATHIBITISHWA

Like
222
0
Thursday, 14 April 2016
Global News

KITUO cha Taifa cha Kudhibiti Magonjwa nchini Marekani (CDC) kimethibitisha kwamba virusi vya Zika husababisha watoto kuzaliwa na vichwa vidogo na ubongo kudumaa.

Hayo yamejiri kufuatia kuwepo kwa mjadala mkubwa na sintofahamu kuhusu uhusiano kati ya virusi hivyo na watoto kuzaliwa na vichwa vidogo tangu kuongezeka kwa visa vya watoto kuzaliwa na vichwa vidogo Brazil.

Mkurugenzi mkuu wa CDC Tom Frieden amesema hakuna shaka kwamba virusi vya Zika vinasababisha watoto kuzalwia na vichwa vidogo, tatizo ambalo kwa Kiingereza hujulikana kama microcephaly.

Comments are closed.