UINGEREZA YAMTAMBUA MTU WA IS

UINGEREZA YAMTAMBUA MTU WA IS

Like
226
0
Tuesday, 05 January 2016
Global News

VYANZO vya kiintelijensia nchini Uingereza vimeiambia BBC kwamba vinaamini wamemtambua mwanaume mwenye asili ya nchi hiyo ambaye anaonekana katika mkanda wa video wa hivi karibuni wenye kupigia chapuo propaganda za kundi la kigaidi la wanamgambo wa Islamic State.

 

Vyanzo hivyo vimemtaja mtu huyo kuwa ni Siddhartha Dhar, ambaye anaaminika alikuwa akiishi Mashariki mwa London.

 

Kwa asili Siddhartha anatajwa kuwa ni Mhindi ambaye aliamua kubadilisha dini yake ya awali na kuwa Mwislamu na inafahamika kuwa baada ya hapo aliamua kujiunga na kundi lenye msimamo mkali la Al Muhajiroun.

Comments are closed.