UINGEREZA YATHIBITISHA KUHUSIKA NA MASHAMBULIZI DHIDI YA IS

UINGEREZA YATHIBITISHA KUHUSIKA NA MASHAMBULIZI DHIDI YA IS

Like
188
0
Thursday, 03 December 2015
Global News

WIZARA ya Ulinzi ya Uingereza imethibitisha kuwa ndege za kijeshi za Uingereza zimetekeleza mashambulio ya angani dhidi ya kundi la Islamic State nchini Syria saa chache baada ya bunge kuidhinisha mashambulio hayo,

Duru za serikali zimesema ndege hizo tayari zimerejea kambini katika visiwa vya Cyprus.

Awali, wabunge nchini Uingereza walikuwa wamepiga kura kwa wingi kuunga mkono mashambulio hayo, wabunge 397 wakiunga mkono dhidi ya 223, baada ya mjadala mkali uliodumu saa 10 katika bunge la Commons.

Comments are closed.