KAMPUNI ya usafiri inayofanya safari zake kati ya Ufaransa na Uingereza ya Eurotunnel imesema maelfu ya wahamiaji wamekuwa wakijaribu kuingia nchini Uingereza kupitia usafiri huo.
Ripoti ya kampuni hiyo imebainisha kuwa idadi ya majaribio ya wahamiaji kutaka kuvuka mpaka kupitia usafiri aina hiyo ya usafiri imeongezeka zaidi, kwani wahamiaji hao wanajificha kwenye magari ya mizigo,kupanda vizuizi.
Katika mkutano wa Mawaziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa na Uingereza uliofanyika mjini London,mbinu za pamoja kuweza kudhibiti wahamiaji hao kuvuka zimejadiliwa na kuelezea hali kuwa ni tatizo kubwa kwa sasa.