UJERUMANI imepanga punguzo la Kodi la Euro Bilioni 1 kuimarisha matumizi mazuri ya Nishati katika majumba na kuongeza biashara ya magari yanayotumia nishati ya umeme, katika mpango wa kusaidia uchumi huo mkubwa katika bara la Ulaya kufikia malengo yake ya utoaji wa gesi zinazochafua mazingira.
Waraka wa Sera ya Nishati umeonesha kwamba licha ya kuelekea katika Nishati Mbadala , utoaji wa gesi zinazoharibu mazingira nchini Ujerumani umepanda kutokana na kuachana na matumizi ya nishati ya kinyuklia.
Baraza la Mawaziri la Kansela ANGELA MERKEL linatarajia kukutana Desemba 3 kukubaliana kuhusu mapendekezo kadhaa kusaidia kujaza pengo, ambalo Mawaziri wanakadiria linafikia asilimia 7, ikiwa ni pamoja na ongezeko la matumizi mazuri ya nishati.