UJERUMANI YAPUUZA WITO WA MAREKANI

UJERUMANI YAPUUZA WITO WA MAREKANI

Like
222
0
Tuesday, 15 December 2015
Local News

WAZIRI wa Ulinzi wa Ujerumani Ursula Von Der Leyen amepuuza wito wa Marekani wa kuitaka Ujerumani kuchangia zaidi kijeshi katika kukabiliana na kundi la wanamgambo wenye itikadi kali wa Dola la Kiislamu IS.

Von Der Leyen amesema Ujerumani tayari inapambana dhidi ya makundi yenye itikadi kali ikiemo nchini Mali na Afghanistan na kuongeza kuwa Ujerumani inatuma ndege za kufanya shughuli za upelelezi nchini Syria zinazohitajika kwa dharura.

Hata hivyo Waziri huyo wa Ulinzi wa Ujerumani amesema ataiandikia Marekani kuifahamisha kuwa inaiunga mkono nchi hiyo katika vita dhidi ya IS.

Comments are closed.