UKAME WAATHIRI SEHEMU KUBWA YA ARDHI YA NCHI

UKAME WAATHIRI SEHEMU KUBWA YA ARDHI YA NCHI

Like
333
0
Thursday, 04 June 2015
Local News

OFISI ya Makamu wa Rais- Mazingira imebainisha kuwa takribani asilimia 61 hadi 75 ya eneo la ardhi ya Tanzania limeathirika na janga la ukame ambao unaweza kusababisha uzorotaji wa shughuli za ukuaji wa uchumi.


Hayo yalielezwa na Afisa Mazingira wa Ofisi ya Makamu wa Rais, ZAINAB SHABAN wakati akitoa mada katika semina ya kukuza uelewa wa masuala ya usimamizi wa mazingira kwa watendaji wa halmashauri ya jiji la Tanga mkoani humo.


Aidha amesema kuwa uchumi wa Tanzania unategemea kwa kiasi kikubwa rasimali asili ikiwemo ardhi, misitu na maji ambapo inakadiriwa asilimia 75 ya wanachi waishio vijijini hutegemea zaidi ardhi katika uendeshaji wa maisha yao.

Comments are closed.