UKAWA WAKUBALIANA KUSIMAMISHA MGOMBEA MMOJA KWENYE KILA KATA NAFASI ZA MADIWANI

UKAWA WAKUBALIANA KUSIMAMISHA MGOMBEA MMOJA KWENYE KILA KATA NAFASI ZA MADIWANI

Like
172
0
Thursday, 13 August 2015
Local News

VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi- UKAWA- Vimesaini Waraka wa Ushirikiano  katika Kugombea nafasi za madiwani kwenye Uchaguzi Mkuu ambapo vitakua na Mgombea mmoja ataewakilisha vyama hivyo kwa kila kata.

 

Waraka huo umesainiwa leo na Makatibu wakuu wa vyama hivyo mbele ya Waandishi wa habari huku Chama cha NLD kikiwakilishwa na Katibu Mkuu Tozzy Matwanga, Chama cha CUF Naibu Katibu Mkuu Magdalena Sakaya, Chama cha NCCR Mageuzi Kaimu Katibu Mkuu Dokta George Kahangwa na CHADEMA Naibu Katibu Mkuu John Mnyika ambapo wamekubaliana Mgombea anayekubalika zaidi ndiye atakaepewa nafasi.

 

 

Comments are closed.