UKAWA WASUSIA MCHAKATO WA KURA YA MAONI KUHUSU KATIBA

UKAWA WASUSIA MCHAKATO WA KURA YA MAONI KUHUSU KATIBA

Like
266
0
Friday, 23 January 2015
Local News

UMOJA wa katiba ya wananchi -UKAWA, umesema kuwa hawatashiriki katika mchakato wa kura za maoni kutokana na mapungufu mbalimbali yanayolikabili zoezi hilo ikiwemo mchakato wa kupata katiba pendekezwa haukuzingatia maridhiano ya kitaifa.

Akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa umoja huo ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha wananchi Cuf Profesa Ibrahim Lipumba amesema kuwa kutokana na mapungufu hayo Ukawa walisusia mchakato huo tangu ulipoanza na pia Rais alipuuza makubakubaliano baina ya umoja wa Demokrasia Tanzania ambao unaundwa na vyama vya siasa vyenye uwakilishi bungeni kuahirisha mchakato wa kura ya maoni hadi baada ya uchaguzi mkuu.

Comments are closed.