UKAWA YAAHIDI KUTATUA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

UKAWA YAAHIDI KUTATUA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

Like
265
0
Friday, 14 August 2015
Local News

CHAMA  cha wananchi- CUF Mkoa wa Morogoro  kimesema kikipata ridhaa ya wananchi kupitia ukawa kitahakikisha kinasimamia migogoro ya wakulima na wafugaji kwa kuweka  bayana mipaka ya vijiji vya wakulima na wafugaji ili kuondoa malalamiko ya muingilano wa shughuli za kilimo na ufugaji.
Akizungumza  kwenye mkutano wa hadhara muda mfupi baada ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la kilosa  kupitia ukawa mwenyekiti wa chama cha wananchi cuf wilaya ya morogoro mjini Abedi Mlapakolo ameeleza idadi kubwa ya wakulima na wafugaji wamepoteza maisha kufuatia mapigano kati yao ambapo amesema mwaka huu ni mwaka wa mwisho kwa wananchi wa kilosa na mvomero kushuhudia mapigano endapo wananchi hao wataamua kufanya mmamuzi magumu.

Comments are closed.