UKAWA YAPINGA MATOKEO NA KUITAKA TUME KUSITISHA ZOEZI

UKAWA YAPINGA MATOKEO NA KUITAKA TUME KUSITISHA ZOEZI

Like
190
0
Wednesday, 28 October 2015
Local News

WAKATI  Tume  ya Taifa ya Uchaguzi nchini-NEC-ikiendelea na Zoezi la kuhesabu kura, vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi-UKAWA- vimeendelea kupinga Matokeo na kuiomba Tume hiyo kusitisha zoezi hilo kwa madai kuwa zoezi hilo halitendi haki kwa vyama vya upinzani.

Hayo yamebainishwa leo na Mgombea wa nafasi ya Uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaeungwa mkono na –UKAWA- Edward Lowasa wakati akizungumz na Waandishi wa habari ambapo amesema ni vyema Tume kuanza upya zoezi hilo kwa kutumia karatasi zilizosainiwa na mawakala na kuacha kutumia mfumo wa IT.

Aidha Lowasa amewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki wakati wakifuatilia matokeo yanayoendelea kutolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Comments are closed.