UKOSEFU WA TAKWIMU SAHIHI UNACHANGIA KUKWAMISHA MIPANGO YA KIMAENDELEO NCHINI

UKOSEFU WA TAKWIMU SAHIHI UNACHANGIA KUKWAMISHA MIPANGO YA KIMAENDELEO NCHINI

Like
309
0
Tuesday, 19 May 2015
Local News

UKOSEFU wa Takwimu sahihi katika Masuala mbalimbali umeelezwa kuchangia kutopiga hatua kwenye mipango ya Kimaendeleo inayopangwa na Serikali juu ya Wananchi.

Aidha upotoshaji wa Takwimu hizo unaofanywa na baadhi ya Watendaji kwa kutaka kujinufaisha wao wenyewe, pia umekuwa ukichangia kuchelewa hatua za Kimaendeleo.

Hayo yameelezwa na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Zanzibar, AMINA SHAABAN,wakati akifungua Semina ya siku moja ya kujadili Malengo ya Millenia baada ya 2015 iliyofanyika mjini hapa.

ZNZ2

Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia hutuba ya Katibu Mtendaji Bi Amina Shabani akifungua mkutano huo.

ZANZ3

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi (ESRF), Dk Oswald Mashindano akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kupitia mafanikio ya Maendeleo ya Malengo ya Millenia MDG’s Tanzania uliofanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini Zanzibar.

 

Comments are closed.