UKRAINE: BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LAHIMIZA MAKUBALIANO YA KUWEKA SILAHA CHINI YAHESHIMIWE

UKRAINE: BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LAHIMIZA MAKUBALIANO YA KUWEKA SILAHA CHINI YAHESHIMIWE

Like
223
0
Wednesday, 18 February 2015
Global News

KUFUATIA mapigano makali katika mji wa Mashariki ya Ukraine,baraza la usalama la Umoja wa mataifa limehimiza makubaliano ya kuweka chini silaha yaheshimiwe haraka.

Muswada wa azimio uliowasilishwa na Urusi umezitaka pande zote zinazohasimiana zitekeleze makubaliano yaliyofikiwa wiki iliyopita mjini Minsk.

Tayari Wanadiplomasia wa nchi za Magharibi wameliangalia azimio hilo kuwa ni ushindi kwa sababu kwa mara ya kwanza mataifa yote 15 Wachama wa Baraza la Usalama wameyatambua matokeo ya mkutano wa Kilele wa Minsk.

Comments are closed.