UKRAINE: BUNGE LAHIDHINISHA HATUA YA KUJIUZULU KWA MWENDESHA MASHTAKA MKUU

UKRAINE: BUNGE LAHIDHINISHA HATUA YA KUJIUZULU KWA MWENDESHA MASHTAKA MKUU

Like
281
0
Tuesday, 29 March 2016
Global News

BUNGE la Ukraine limeidhinisha hii leo hatua ya kujiuzulu kwa mwendesha mashtaka mkuu nchini humo Viktor Shokin mtu ambaye amekuwa akionekana na nchi za magharibi zinazoiunga mkono Ukraine kama kizingiti katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi.

Marekani imekuwa mara zote ikitaka pafanyike mageuzi kuanzia ngazi za juu katika ofisi hiyo ya mwendesha mashaka.

Hata hivyo Wanaharakati wanaopinga rushwa wamekuwa wakisema kwamba ofisi ya mwendesha mashitaka huyo mkuu imekuwa na dhima muhimu katika kuyalinda maslahi ya wala rushwa na kuruhusu kushamiri kwa vitendo vya ulaji rushwa na ufisadi.

Comments are closed.